• Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Barua za Watumishi |
    • Malalamiko/mrejesho |
Nachingwea District Council
Nachingwea District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Mikakati
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii Vijana na Ustawi wa Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Sekondari
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Mkaguzi wa ndani
      • Uchaguzi
      • TEHAMA
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Ugani
  • Madiwanii
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Utawala Mipango na Fedha
      • Ujenzi uchumi na mazingira
      • Huduma za Jamii
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa madiwani
      • Ratiba ya kuonana na mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Fomu
    • Sheria
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari

FURSA ZA UFUGAJI NACHINGWEA

Start Date: 2022-02-01
End Date: 2023-02-01

 

 

 

 MIFUGI NA UVUVI

 

Wilaya ya Nachingwea haina wafugaji wengi kwakuwa toka miaka ya nyuma makabila ya maeneo haya hawakuwa na utamaduni wa ufugaji.

Mifugo iliyokuwa inafugwa ni jamii ya ndege ambao nao walikuwa wanafugwa kwa kiwango kidogo tu kwa matumizi ya nyumbani

Kwa sasa jamii ya watu wa Nachingwea wameanza kuhamasika kufuga hasa baada ya kuona matokeo ya utekelezaji wa miradi mbalimbali kama RIPS,WFP,HPI na DADPS ambayo ilijishughulisha na kuhamasisha shughuli za maendeleo ikiwemo ufugaji wa ng’ombe wa maziwa,mbuzi,nguruwe na kuku

Kwa sasa wilaya ina jumla ya ng’ombe 11,273, Mbuzi 11,625, Kondoo 1409, Nguruwe 3235, Mbwa 3281 na kuku 324,200

Fursa zilizopo katika kuendeleza ufugaji:

 

Hali ya hewa-Hali ya hewa ni rafiki kwa ufugaji wa aina mbalimbali za mifugo jambo ambalo litaruhusu uzalishaji bora wa mifugo na mazao yake

Nyanda za malisho - Wilaya ya Nachingwea ina jumla ya vijiji 25 vilivyofanyiwa mpango wa matumizi bora ya ardhi na kati ya hivyo,vijiji 23 vimetenga maeneo ya malisho ya mifugo ambapo jumla ya Hekta 61,604 zimetengwa ambapo hekta 49,795.46 zenye uwezo wa kupokea ng’ombe 24,897 zilitengwa kwa ajili ya wafugaji wahamiaji katika vijiji vya Mtua,Chimbendenga,Mbondo,Kilimarondo,Kiegei B,Namatunu na Matekwe na hekta 11,808.54 ni kwa ajili ya wafugaji wa ndani kwenye maeneo mengine ya wilaya.Uwepo wa masalia ya mazao ya mashambani nao unachangia kwa kiwango cha kutosha katika kuongeza malisho ya mifugo

 

Uwepo wa magonjwa machache ya mifugo-Ukanda huu wa kusini una magonjwa machache sana ya mifugo ikilinganishwa na maeneo mengine jambo ambalo ni fursa adhimu katika kuendeleza sekta ya ufugaji kwa kuwa kutakuwa na ustawi wa kutosha kwa mifugo

Soko la mazao ya mifugo-Kutokana na uchache wa mifugo uliopo kwa sasa, mahitaji ya mazao ya mifugo kwa wananchi ni makubwa hivyo kuna uhakika wa soko la mazao yatokanayo na mifugo

Uzalishaji na masoko ya mazao ya mifugo:

 

Tasnia ya maziwa: 

Aina ya mnyama
Waliokamuliwa

Uzalishaji

(lita)

Wastani wa bei kwa lita (T.shs)

Thamani

(T.shs)

Ng’ombe

248

323,632

1,500

485,448,000

Mbuzi

0

0

0

0.00

Jumla 

248

323,632

1,500

485,448,000

 Tasnia ya nyama:

Aina ya mifugo

Idadi chinjwa 

Wastani wa uzitokwa mnyama (kg)

Jumla ya kilo za

Nyama

Bei kwa

kilo (T.shs)

Thamani ya nyama(T.shs)


Ng’ombe

2,243

100

224,200

8,000

1,793,600,000


Mbuzi/
Kondoo

71

12

852

9,000

7,668,000


Nguruwe

322

45

14,490

8,000

115,920,000


Jumla kuu

2,636

-

-

-

1,917,188,000


 

Mayai: 

Uzalishaji wa mayai ndani ya wilaya katika kipindi hiki unakadiriwa  kuwa kama ifuatavyo:

Aina ya kuku

Idadi ya watagaji

Idadi ya mayai      tagwa

Wastani wa bei/yai (TZS)

Thamani

(TZS)

Kuku wa asili

112,400

1,686,000

500

843,000,000

Kuku wa mayai

1,740

628,600

500

314,300,000

Jumla 

114,140

2,314,600

500

1,157,300,000

 

 Tasnia ndogo ya uvuvi: 

  • Wilaya ya Nachingwea kijiografia haina Bahari, Maziwa wala Mito ya kudumu ambayo ingeweza kuzalisha samaki wa aina mbalimbali. Hata hivyo katika jitihada za kuendeleza sekta ya uvuvi,wilaya imekuwa  ikitumia mabwawa madogo yaliyoachwa na wakoloni kwenye baadhi ya vijiji kama fursa ya kuzalisha Samaki kwenye vijiji hivyo chini ya usimamizi wa Halmashauri za vijiji.
  • Kutokana na changamoto hii, Halmashauri inaendelea kuhamasisha watu binafsi na vikundi kuchimba Mabwawa ya Samaki katika maeneo yao kwa lengo zima la kuboresha lishe kwa kuongeza ulaji wa samaki lakini pia kuongeza kipato kwa kuuza samaki wa ziada.
  • Mpaka sasa wilaya ina jumla ya mabwawa 21 ya samaki, kati ya hayo ,mabwawa 2  yanamilikiwa na vikundi katika maeneo ya  Ugawaji na Uhindini, 1 linamilikiwa na Halmashauri ya kijiji Naipingo na 18 yanamilikiwa na watu binafsi katika maeneoyaMatangini,Stesheni,Mitumbati,Songambele,Ruponda,Chemchemu,Boma mashariki na Naipanga
  •  

  Changamoto zinazoikabili sekta ya mifugo na uvuvi:

Halmashauri ya wilaya Nachingwea inakabiliwa na changamoto mbalimbali katika kutekeleza majukumu ya sekta ya mifugo na uvuvi.Miongoni mwa changamoto hizo ni :

 

  • Upungufu wa wataalam wa mifugo na uvuvi ni moja ya changamoto zinazo zorotesha utendaji katika kutoa huduma za ugani hapa wilayani.Wilaya ina wataalam 15 tu wa mifugo,haina daktari wa mifugo na haina mtaalam wa uvuvi.

                Halmashauri wakati mwingine inatumia vikundi na Redio ya Nachingwea FM katika kuelimisha wananchi juu ya masuala ya ufugaji                          

 

  • Uchakavu wa vitendea kazi kama pikipiki-Hii ni kutokana na ukweli kwamba pikipiki nyingi ni za muda mrefu lakini halmashauri inajitahidi kutenga fedha kwa ajili ya matengenezo ya vyombo vya usafiri zikiwemo pikipiki
  • Ushiriki mdogo wa viongozi wa vijiji katika kusimamia miradi ya ufugaji kwenye maeneo yao.Halmashauri inaendelea kuhamasisha viongozi kushiriki na kusimamia kikamilifu miradi ya ufugaji inayoendelea kwenye maeneo yao
  • Ukosefu wa vyanzo vya kudumu vya maji ya kunyweshea mifugo hususani kwenye maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya mifugo.Halmashauri inaendelea kuhamasisha wafugaji waliopo kuona umuhimu wa kuchimba malambo au visima virefu kwa ajili ya maji ya kunywesha mifugo yao

Matangazo

  • ORODHA YA WANAOITWA KWENYE MAFUNZO YA ANWANI ZA MAKAZI March 26, 2022
  • TANGAZO LA AJIRA WATENDAJI WA KIJIJI III NAFASI 16 NA DERAVA DARAJA II NAFASI NNE May 25, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WALIOOMBA AJIRA ZA UTENDAJI WA KIJIJI NA UDEREVA HALMASHAURI YA WILAYA YA NACHINGWEA July 22, 2022
  • Tangazo la kazi za muda December 27, 2019
  • Angalia zote

Habari mpya

  • WANAFUNZI WA NACHINGWEA HIGH NA RUGWA BOYS WAAGWA KWA HAFLA FUPI, WAJIANDAA KWA MITIHANI YA TAIFA

    April 26, 2025
  • SDA NA LIIKE WATOA MAFUNZO YA HUDUMA YA KWANZA KWA MANGALIBA NA WALOMBO KWA AJILI YA KUIMARISHA UTAMADUNI SALAMA

    April 28, 2025
  • DED NACHINGWEA : AAGIZA MIRADI KUKAMILIKA KWA WAKATI NA KWA KUZINGATIA VIWANGO

    April 09, 2025
  • RC LINDI : MIRADI YOTE ITAKAYOPITIWA NA MWENGE IZINGATIE MATUMIZI BORA YA FEDHA

    April 05, 2025
  • Angalia zote

Video

Wakulima wasisitizwa kulima mazao ya chakula
Video za mpya

Kurasa za Haraka

  • Opras Form
  • Mkurugenzi wa Halmashauri ya Nachingwea Eng. Chionda Alli Mfaume akizungumza waluu wa idara
  • MRADI WA MAJI NAMIKANGO WAZINDULIWA
  • Mpango wa Bajeti
  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2021
  • UANZISHWAJI WA BLOCK FARMING WANANCHI WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA
  • MRADI WA MAJI WA ZAIDI YA BILIONI 1 WAANZA KUTEKELEZWA NAIPANGA
  • Sheria za Fedha za Mitaa
  • Sheria za Halmashauri

Tovuti mashuhuri

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • TUZO ZA ELIMU WILAYA YA NACHINGWEA
  • Utumishi
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao

Idadi ya Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.